• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali |
    • Barua Pepe |
Mtwara District Council
Mtwara District Council

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Mtwara

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Elimu ya sekondari
      • Elimu Msingi
      • Usafi na Mazingira
      • Maji na Umwagiliaji
      • Fedha na Biashara
      • Kazi na Kikosi cha Zima Moto.
      • Maendeleo ya Jamii,Jinsia na Vijana
      • Ardhi,Maliasiri na Mazingira
      • Utawala
      • Mipango,Takwimu na Ufuatiliaji
      • Kililmo na Ushirika
      • Mifugo na Uvuvi
    • Vitengo
      • Kitengo cha Sheria
      • Kitengo cha Uchaguzi
      • Kitengo cha Ugavi
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Habari na Mawasiliano.
    • Kamati za Halmashauri
      • Kamati ya Elimu,Afya na Maji
      • Kamati ya Fedha,Utawala na Mipango
      • Kamati ya Uchumi,Kazi na Mazingira
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Uwekezaji
    • Agriculture
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Huduma za kijamii
    • Huduma za Kifedha
    • Usambazaji Nishati ya Umeme
    • Maji
  • Madiwani
    • Kata ya Nanguruwe
    • Kata ya Mbawala
    • Kata ya Naumbu
    • Kata ya Ziwani
    • Kata ya Libobe
    • Kata ya Mayanga
    • Kata ya Ndumbwe
    • Kata ya Dihimba
    • Kata ya Mkunwa (HQ)
  • Miradi
    • Miradi Mpya
      • On going Project
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Utaratibu
    • Ripoti
    • Sheria
    • Fomu
    • Zabuni
    • Newsletter
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Tukio

Naumbu Msangamkuu zanufaika ziara ya DC

Posted on: July 1st, 2020


Na Afisa habari.

Kata za naumbu na msangamkuu halmashauri ya wilaya ya mtwara jana 30 Juni, 2020 zimepata mashine mbili za boti za uvuvi na nguvu ya kuendelea na ujenzi wa miradi ya maendeleo kwenye sekta ya afya na elimu mara baada ya kutembelewa na mkuu wa wilaya ya mtwara Ndg. Dunstan Kyobya.

Ziara hiyo imeleta neema katika kijiji cha mgao mara baada ya mkuu wa wilaya kukabidhi mashine ya boti ya uvuvi aina ya Yamaha “Horse Power 40” yenye thamani ya milioni 7.5 kwa kikundi cha vijana cha JIWEZESHE kinachofanya shughuli zake katika eneo hilo, mashine hiyo imetolewa kama ruzuku na wizara ya uvuvi ikiwa ni ahadi waliyopewa na kufuatiliwa na ofisi ya mbunge, wanakikundi wamefurahishwa na ruzuku hiyo na kuahidi kutoa ushirikiano na serikali.

“Kwakweli sisi tunashukuru sana, tunaishukuru serikali kwa kutupatia mashine hii na fedha taslimu laki tano kutoka kwa mbunge, pia halmashauri ilitupatia mkopo wa vijana wa Tzs. 13,000,000/= kutokana na hayo tukaacha kabisa uvuvi haramu, sasa hivi tunashirikiana bega kwa bega na serikali” alisema ndg. Ali Juma Salumu Katibu wa kikundi.

Aidha, viongozi hao wameunga mkono ujenzi wa jengo la wazazi katika zahanati ya Mgao ambapo kijiji kina jumla ya Tzs. 10,000,000/= huku mbunge akiwaongezea milioni moja, ujenzi huo unatarajiwa kuanza wiki hii kutokana na uhitaji wa jengo hilo.

Kwa mujibu wa kaimu mkurugenzi mtendaji ndg. Maisha S. Mtipa amesema kuwa, anapongeza juhudi za wananchi pia halmashauri itasaidia kuongeza nguvu zake katika hatua za umaliziaji kwakuwa imetenga kiasi cha fedha kuunga mkono juhudi za wananchi katika miradi kama hiyo.

“Hatuwezi kuacha juhudi za wananchi zipotee bure, kwakuwa mwaka wa fedha 2020/2021 kuna zaidi ya milioni 200 zimetengwa kwaajili ya kusaidia miradi ya nguvu za wananchi kwahiyo tutawaunga mkono ila kwa sasa waanze” aliongea Maisha Mtipa.

Wakati huo huo, mashine ya pili imetolewa kwa kikundi cha MWENDOKASI kinachofanya shughuli za uvuvi katika pwani ya msangamkuu, mwenyekiti wa kikundi hicho ndg. Mzee Musa Malango ameeleza kwamba mapokezi ya mashine hiyo imetegua kitendawili cha muda mrefu kilichokuwa kinawasumbua miongoni mwa vijana kwakuwa wengi wao walihisi haitatekelezwa.

Katika hali isiyo tarajiwa wakati mkutano unaendelea aliibuka mwananchi mmoja aliyemuomba mkuu wa wilaya asimamie harambee ya ujenzi wa shule ya sekondari, harambee hiyo ya dakika 20 ilifanikiwa kupatikana kwa jumla ya Tzs. 1,810,000/=, tofali 2000 na mifuko 50 ya saruji kutoka kwa Mkuu wa wilaya kisha michango ikakabidhiwa kwa mwenyekiti wa kijiji.



Matangazo

  • Orodha ya waliopangiwa kujiunga Kidato cha Kwanza 2019, WAVULANA December 16, 2018
  • Orodha ya waliochaguliwa kujiunga kidato cha kwanza 2019, WASICHANA December 17, 2018
  • Changamkia Fursa ya Viwanja Vilivyopimwa Kwa bei nafuu December 27, 2018
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI WATENDAJI WA VIJIJI na MADEREVA February 26, 2018
  • Angalia Zote

Habari Mpya

  • Mtwara DC kufungua sekondari 4 mpya Januari Mwakani

    December 07, 2020
  • Wanaoanzisha migogoro ardhi wapigwa “stop"

    July 06, 2020
  • Naumbu Msangamkuu zanufaika ziara ya DC

    July 01, 2020
  • Halmashauri yapewa wiki mbili kukamilisha madarasa 15

    June 27, 2020
  • Angalia Zote

Video

RC Mtwara ataka mabadiliko Ligula Hospitali
Video zaidi

Kurasa za Haraka

  • New Projects
  • Speeches
  • Organizational Structure
  • Tenders
  • Applications Forms

Kurasa Mashuhuri

  • Tanzania Government Website
  • PO-RAG
  • Public Service Management
  • Mtwara Region Office
  • Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma
  • Tovuti ya Ikulu

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani ya Sehemu

Wasiliana nasi

    Mtwara.

    Anuani ya posta: 528.

    Simu ya Mezani: 023-2333928

    Simu: 023-2333928

    Barua pepe: Mtwaradc@mtwara.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Usiri
    • Kanusho
    • Maswali
    • Ramani ya Tovuti
    • Huduma

Copyright ©2020 MTWARA DC . All rights reserved.