Na. Afisa Habari
Mkurugenzi mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Mtwara Bi. Erica E. Yegella Leo Tarehe 07 Disemba, 2020 amewaeleza Waheshimiwa Madiwani adhma ya Halmashauri kufungua Shule 4 za Sekondari ifikapo Januari, 2021 kwa lengo la kupunguza kero ya kutembea umbali mrefu kwa Wanafunzi.
Ameyasema hayo katika Kikao Cha Baraza la Madiwani wakati akitoa utangulizi wa uwasilishaji wa taarifa ya utekelezaji uliofanyika kipindi chote ambacho Waheshimiwa hawakuwepo Mara baada ya kuvunjwa kwa Baraza mwishoni mwa Mwezi Juni Mwaka huu ili kupisha mchakato wa Uchaguzi Mkuu uliofanyika Mwezi Oktoba 28.
Akiendelea kutolea ufafanuzi wa ujenzi wa Shule hizo, Bi. Yegella ametanabaisha kuwa vifaa mbalimbali vimeshakwenda katika maeneo ya ujenzi ambapo mafundi wapo kazini na vingine vinaendelea kupelekwa kwa kadri vinapohitajika lengo likiwa kumaliza kwa wakati.
Ameendelea kuzitaja Shule hizo ni kuwa Sekondari ya Tangazo, Lipwidi, Msangamkuu na MangoPachanne, amewaomba Waheshimiwa kuendeleza nguvu ya uhamasishaji ili kufanikisha utekelezaji wa Ilani na Mipango ya maendeleo kwa Wananchi.
Mtwara.
Anuani ya posta: 528.
Simu ya Mezani: 023-2333928
Simu: 023-2333928
Barua pepe: Mtwaradc@mtwara.go.tz
Copyright ©2020 MTWARA DC . All rights reserved.